Sunday, 30 June 2019
#ENEWS:Indigo Ya Chris Brown Kuangukia Nafasi Ya 1 Billboard.Tazama Mauzo
Album mpya ya Chris Brown inatarajiwa kushika namba moja kwenye chati za wiki ijayo za Billboard 200 ikiwa na maana ya album iliyouza zaidi wiki hii. Kwa mujibu wa Hits DailyDouble, Indigo inatarajiwa kuuza kati ya Nakala 110,000 na 135,000 ndani ya wiki ya kwanza.
Kama Album itauza kama inavyotarajiwa basi Hii itakuwa Album ya Tatu ya Breezy kushika namba 1 kwenye “Billboard 200”, Album yake iliyopita “Heartbreak on A Full Moon” ilidondokea namba Tatu kwenye chati hizo.
Album ya “Indigo” imewashirikisha wakali wengine kama Drake, Justin Bieber, Tory Lanez, HER, Nicki Minaj, Lil Wayne, na Trey Songz.
Labels:
Entertainment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment