Tuesday, 9 July 2019

VIDEO | Nandy - Mimi ni wa juu (Cover song)

Watch/Download Mimi Ni Wa Juu Video By Nandy 



VIDEO | Harmonize X Milly Nanace - Never Give Up REMIX (Official Video)

Watch /Download Never Give Up Video Remix By Harmonize and Milly Nanace 



VIDEO | Machine Gun Kelly, Trippie Redd - Candy (Official Video)

Watch/Stream Candy Video By Machine Gun Kelly and Trippie Redd


Candy inapatikana kwenye album mpya ya Machine Gun Kelly, 'Hotel Diablo' iliyotoka week iliyopita.Ndani ya video anaonekana rafiki yake wa karibu ambaye ni member wa FNL, Comedian Peter Davidson.Itazame hapo chini


#MAPENZI:Yajue Haya Muhimu Kabla Ya Kuingia Kwenye Ndoa

Ni vizuri ukaiandaa akili yako kabla haujafanya maamuzi sahihi yatakayopelekea maisha yako kuwa na furaha au kilio hapo baadaye kwa yule uliyemchagua kuwa naye.

Ila tabia na mambo hayo hapo chini huwa yanabadilika kuendana na wakati na sio kila binadamu hawezi kubadilika kitabia, wapo wanaoweza kubadilika pia.

YAJUE HAYA
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.

2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada
ya Ndoa.(Inategemeana na mtu pia ila sio kwa wote)

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu
yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi
fanywa na mtu yeyote.

5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na
Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama
kuolewa na mtu hasiye sahihi.

7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.(Katika hili pia sio wote ambao ni wa kuepukwa wengine ni mapungufu yao na wakipata ushauri mzuri hubadilika)

8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe
na Ndoa yenye furaha.

9. Maneno matatu yanayojenga amani katika
Ndoa:
a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante.

10. Kupiga punyeto ni kujiharibu.

11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga
bila jua.

12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
Mungu mmoja - Mume mmoja - Mke mmoja.

13. Furaha ya kudumu maisha hutegemea na
chaguo lako la Ndoa.

14. Usioe pesa au mali - muoe mtu.

15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa
isiyo na amani na furaha.

16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano
mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke
mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama
kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa kigezo
tu anakidhi haja zako kingono.

18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki
wema.

19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.

20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza…

MUHIMU.Zingatia haya na utapata furaha na amani katika ndoa yako baada ya kufanya maamuzi na chaguo sahihi la yule utakayekwenda kuishi naye.

#AFYA:Faida Za Kula Mayai Wakati Wa Asubuhi

Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. 
Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai.

Zifuatazo ndizo faida  za kula mayai wakati wa Asubuhi;

1. Hutunza shibe

Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.

2. Husaidia kupunguza uzito
Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.

3. Mayai ni bei rahisi
Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.

4. Mayai ni chanzo kikubwa cha protini
Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.

Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.

5. Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)
Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.

6. Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu
Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.

7. Hulinda macho
Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.

Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.

#AFYA:Vyakula Vinavyoongeza Uwezo Wa Kuona

Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.
Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.

Samaki

Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.

Mboga za majani
Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.

Mayai
Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).

Matunda jamii ya mchungwa na zabibu
Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.

Karanga na jamii zake
Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.

Matunda ya rangirangi
Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.

Vyakula vya jamii ya kunde
Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.

Alizeti
Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.

Nyama ya ng’ombe
Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.

Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.