Wednesday, 10 July 2019
Tuesday, 9 July 2019
VIDEO | Nandy - Mimi ni wa juu (Cover song)
VIDEO | Machine Gun Kelly, Trippie Redd - Candy (Official Video)
Watch/Stream Candy Video By Machine Gun Kelly and Trippie Redd
Candy inapatikana kwenye album mpya ya Machine Gun Kelly, 'Hotel Diablo' iliyotoka week iliyopita.Ndani ya video anaonekana rafiki yake wa karibu ambaye ni member wa FNL, Comedian Peter Davidson.Itazame hapo chini
#MAPENZI:Yajue Haya Muhimu Kabla Ya Kuingia Kwenye Ndoa
Ni vizuri ukaiandaa akili yako kabla haujafanya maamuzi sahihi yatakayopelekea maisha yako kuwa na furaha au kilio hapo baadaye kwa yule uliyemchagua kuwa naye.
Ila tabia na mambo hayo hapo chini huwa yanabadilika kuendana na wakati na sio kila binadamu hawezi kubadilika kitabia, wapo wanaoweza kubadilika pia.
YAJUE HAYA
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada
ya Ndoa.(Inategemeana na mtu pia ila sio kwa wote)
3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.
4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu
yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi
fanywa na mtu yeyote.
5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na
Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.
6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama
kuolewa na mtu hasiye sahihi.
7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.(Katika hili pia sio wote ambao ni wa kuepukwa wengine ni mapungufu yao na wakipata ushauri mzuri hubadilika)
8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe
na Ndoa yenye furaha.
9. Maneno matatu yanayojenga amani katika
Ndoa:
a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante.
10. Kupiga punyeto ni kujiharibu.
11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga
bila jua.
12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
Mungu mmoja - Mume mmoja - Mke mmoja.
13. Furaha ya kudumu maisha hutegemea na
chaguo lako la Ndoa.
14. Usioe pesa au mali - muoe mtu.
15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa
isiyo na amani na furaha.
16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano
mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke
mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.
17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama
kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa kigezo
tu anakidhi haja zako kingono.
18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki
wema.
19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.
20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza…
#AFYA:Faida Za Kula Mayai Wakati Wa Asubuhi
Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao.
Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai.
Zifuatazo ndizo faida za kula mayai wakati wa Asubuhi;
1. Hutunza shibe
Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.
2. Husaidia kupunguza uzito
Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.
3. Mayai ni bei rahisi
Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.
4. Mayai ni chanzo kikubwa cha protini
Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.
Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.
5. Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)
Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.
6. Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu
Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.
7. Hulinda macho
Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.
Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.
1. Hutunza shibe
Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.
2. Husaidia kupunguza uzito
Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.
3. Mayai ni bei rahisi
Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.
4. Mayai ni chanzo kikubwa cha protini
Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.
Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.
5. Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)
Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.
6. Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu
Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.
7. Hulinda macho
Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.
Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.
#AFYA:Vyakula Vinavyoongeza Uwezo Wa Kuona
Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.
Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.Samaki
Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.
Mboga za majani
Mboga za majani
Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.
Mayai
Mayai
Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).
Matunda jamii ya mchungwa na zabibu
Matunda jamii ya mchungwa na zabibu
Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.
Karanga na jamii zake
Karanga na jamii zake
Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.
Matunda ya rangirangi
Matunda ya rangirangi
Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.
Vyakula vya jamii ya kunde
Vyakula vya jamii ya kunde
Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.
Alizeti
Alizeti
Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.
Nyama ya ng’ombe
Nyama ya ng’ombe
Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.
Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
#ENEWS:Chris Brown Atoa Shukrani Baada Ya Jambo Hili Kubwa Kufanikiwa
Msanii Chris Brown ametoa shukrani kwa mashabiki pamoja na mtandao wa Billboard baada ya album yake, Indigo kufanikiwa kuingia nafasi ya 1 katika chart 200 za album bora kwa mauzo ya week ya kwanza ambayo yamegonga 108,000.
Breezy ametumia mitandao yake ya kijamii kutoa shukrani hizo.
Indigo album imecontain ngoma 32 na imeshirikisha wasanii wakali kama Drake, Nicki Minaj, Lil Wayne, Tyga, Tory Lanez na wengine.
Top 10 Album Ndani Ya Billboard Week Hii
BILLBOARD 200 TOP 10
1. Chris Brown – Indigo – 108,000
2. Lil Nas X – 7 – 62,000
3. Billie Eilish – When We All Fall Asleep, Where Do We Go? – 52,000
4. The Black Keys – Let’s Rock – 52,000
5. Chance the Rapper – Acid Rap – 40,000
6. Khalid – Free Spirit – 38,000
7. Lizzo – Cuz I Love You – 36,000
8. Mustard – Perfect Ten – 36,000
9. J Balvin and Bad Bunny – Oasis – 36,000
10. Jonas Brothers – Happiness Begins – 29,000
2. Lil Nas X – 7 – 62,000
3. Billie Eilish – When We All Fall Asleep, Where Do We Go? – 52,000
4. The Black Keys – Let’s Rock – 52,000
5. Chance the Rapper – Acid Rap – 40,000
6. Khalid – Free Spirit – 38,000
7. Lizzo – Cuz I Love You – 36,000
8. Mustard – Perfect Ten – 36,000
9. J Balvin and Bad Bunny – Oasis – 36,000
10. Jonas Brothers – Happiness Begins – 29,000
#ENEWS:August Alsina Apelekwa Hospitalini (VIDEO)
August Alsina amerudishwa tena hospitali baada ya kupoteza uwezo wa kutembea. Mwimbaji huyo amewapa taarifa hiyo mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram.
Tatizo linalomsumbua Alsina ni Ini ambalo linapelekea kinga ya mwili kushindwa kupambana. Kwenye video aliyoiweka kwenye akaunti yake ya instagram amesikika akisema anaomba radhi kwa kushindwa kutumbuiza kwenye tamasha la Essence juzi Jumapili. Pia amewapa tumaini kuwa atakuwa salama na kurejea kwenye hali yake.
TAZAMA VIDEO VIA INSTAGRAM HAPO CHINI
Hiiii guys!! 😂It's me, being my most awesome, weirdly great self. 🤦🏽♂️I'm here with the stitch 🗣 & to also apologize for not being able to make the essence fest gig last night. I take my career & your time very seriously & the fact that you guys show up for me, endlessly. Means the world! I'm man down right now, & figured I should share.. that My auto immune disease is raging, but im fighting this thing & on my mission to shake back & beable to make it up to you! I got so much 🎶NEW NEW🎶 to share w/ you!!!..& Big Love to give. ❤️ Big Life, Big Dreams & every peaceful thing to you! Less stress, More Love, More Rest, & Jah Bless. 🙏🏽 know that HE's got you even when it all feels too complex. 👁⚡️🙏🏽
190.1k Likes, 16.8k Comments - Yungin' (@augustalsina) on Instagram: "Hiiii guys!! 😂It's me, being my most awesome, weirdly great self. 🤦🏽♂️I'm here with the stitch 🗣 &..."
AUDIO | Lameck Ditto - Nikuone (Official Audio)
#TEKNOJIA:Kosa Kubwa Analolijutia Billionaire Bill Gates
Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amenukuliwa akisema kuwa katika moja ya kosa lake kubwa la wakati wote alilolifanya ni kuiacha Android kuongoza katika mifumo ya uendeshaji Duniani.
Amesema katika ulimwengu wa programu anayeongoza katika kuwa na programu endeshaji inayotumika kwenye vifaa vingi zaidi ndiye anakuwa mshindi wa masoko yote. Hivyo kwa upande wa Microsoft imefanya kosa kubwa ambalo limeifanya Android kuongoza sokoni.
Android kwa sasa ndio mfumo endeshi unaoongoza kwa kutumiwa na watu wengi zaidi duniani ukifuatiwa na mfumo wa Microsoft, yaani Windows.
Mfumo Wa Android ndyo mfumo ulio na watumiaji wengi duniani kwa wakati huu ukitofautishwa na kipindi cha nyuma ambacho Blackberry ndyo walikuwa wamelishika soko.
Microsoft ilijaribu kuleta programu endeshaji spesheli kwa ajili ya simu iliyokwenda kwa jina la Windows Mobile kwa upande wa simu zake za Windows Phone lakini haikupokelewa vizuri sokoni na pia kwa watengenezaji wa apps. Microsoft ikajikuta bado inabaki ikitamba katika kompyuta zaidi.
AUDIO | Mo Music Ft Atan Voice – Niseme Nae (Official Audio)
#SPORTS:Tunisia Yatinga Robo Fainali Afcon 2019, Ivory Cost Kunani...?
Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.
Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.
Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza.
Kwa Upande mwingine Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon.
Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi.
Monday, 8 July 2019
#SPORTS:Jose Morinho Apiga Chini Dili LA China
Jose Mourinho amekataa ofa ya kwenda kufundisha nchini China.
Mourinho amehusishwa na taarifa za kufuatwa na timu ya Guangzhou Evergrande akipewa ofa ya kitita cha pauni milioni 88.
Donge hilo lingemfanya kuwa kocha anayelipwa fedha nyingi duniani lakini Mourinho ametaka kuendelea kubaki Uingereza na familia yake.
Mourinho hajawa kazini tangu alipofukuzwa na Manchester United mwaka jana mwezi Disemba.
Guangzhou kwa sasa wanafundishwa na kocha muitaliano Fabio Cannavaro.
Mourinho alisema mwezi Machi kuwa anataka kurejea kwenye kazi yake ya ukocha mwakaa huu, lakini anasubiri kazi itakayomfaa.
''Ninajua kwa hakika nisichokitaka,'' alisema.
''Ninajua ninachokitaka, si timu fulani lakini namna ya kazi ilivyo na ukubwa wa kazi.''
#SPORTS:Taarifa Ya Kuvunjika Kwa Mkataba Wa Kocha Wa Taifa Stars
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limethibisha kuachana na kocha timu ya taifa 'Taifa Stars', Emmanuel Amunike kwa makubaliano ya baina ya pande mbili.
Uamuzi wa TFF umekuja wakati kukiwa na presha kubwa ya wadau wa soka nchini wakishindikiza Amunike hatimuliwe tangu Tanzania ilipofuzu kwa mara ya kwanza kwa Afcon Aprili na baada ya mashindano hayo yanayoendelea Misri.
Katika mashindano ya Afcon2019, Tanzania ikiwa Kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya ilipoteza mechi zote na kuambulia pointi tatu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo kupitia kwa Ofisa Habari wake, Cliford Ndimbo imesema shirikisho na kocha wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba baina yao.
Alisema shirikisho litatangaza kocha wa muda ambaye atakiongoza kikosi cha timu ya taifa kinachotarajia kushiriki mashindano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
"Makocha wa muda watatangazwa baada ya kamati ya dharura ya kamati ya utendaji (Emergency Committee) itakayofanyika Julai 11 mwaka huu," ilisema taarifa ya Ndimbo na kuongeza kuwa mchakato wa kutafuta kocha mpya umeshaanza.
ENEWS:Diamond Platnumz Athibitisha Tanasha Ana Ujauzito Wake (PICHA)
Msanii Diamond Platnumz amethibitisha kuwa mpenzi wake Tanasha Donna ana ujauzito wake na jinsia ya mtoto huyo ni wa kiume kwani tayari walishaenda kufanya checkup ya vipimo.
Diamond ametumia picha walizopiga tarehe ya kuzaliwa ya mpenzi wake huyo siku ya July 7 na kuweka kwenye akaunti yake ya instagram na caption inayosomeka, "Alhamdulilah, it's a BOY! 👶 @tanashadonna ❤...."
Tanasha Donna amesheherekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na B Sadra ambaye ni mama yake Diamond Platnumz ambapo shughuli maalumu ilifanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kupewa jina la The Great Gastsby.
VIDEO | Tyga - Lightskin Lil Wayne (Official Video)
Watch/Stream Lightskin Lil Wayne Video By Tyga
Rapper Tyga ameileta video ya Lil Wayne Lightskin ikiwa inaonyesha baadhi ya scene za nyimbo alizoimba Weezy huku yeye akiigiza kama Wayne, ndyo maana kamili ya wimbo huo.Utazame hapo chini
VIDEO | Ed Sheeran Ft Bruno Mars & Stepleton - Blow (Official Video)
Watch/Stream Blow Video By Ed Sheeran Featuring Bruno Mars
Tarehe 12 July Album ya Ed Sheeran, No.6 Collaborations Project inategemewa kuingia sokoni, Blow ni moja kati ya ngoma ambayo itakuwemo ndani.Right now itazame video yake
Sunday, 7 July 2019
VIDEO | Soft - Money (Remix) ft. Wizkid (Official Video)
VIDEO | Christian Bella Ft AY& Mwana FA - Pete (Official Video)
Watch/Download Pete Video By Christian Bella Featuring Mwana FA & AY
DOWNLOAD VIDEO|MP4
DOWNLOAD AUDIO|MP3
AUDIO | Christian Bella Ft AY& Mwana FA - Pete (Official Audio)
#SPORTS:Lampard Aahidi Hili Na Kuwaambia Wachezaji Wake...
Kocha mpya wa Chelsea, Frank Lampard amewaambia wachezaji wake tena kwa msisitizo kwamba ni lazima wamalize ndani ya Top Four kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.
Wababe hao wa Stamford Bridge kwa sasa wanakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kusajili kwa kipindi cha miaka miwili, lakini wamefanikiwa kumbakiza kiungo Mateo Kovacic kwenye kikosi chao baada ya kumbeba jumla kutoka Real Madrid kufuatia mkataba wake wa mkopo kufika mwisho.
Chelsea waliwalipa Madrid Pauni 40 milioni ili kunasa huduma ya Kovacic moja kwa moja, aendelee kuwapo kwenye kikosi chao kwa ajili ya mapambano ya kwenye Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kwenye dirisha la usajili wa Januari, Chelsea walinasa huduma ya Christian Pulisic kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya Pauni 58 milioni na kisha kumbakiza kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Ujerumani, lakini sasa atajiunga na wababe hao wa Stamford Bridge katika dirisha hili.
Lampard alisema: "Nimecheza hapa kwa miaka mingi, nafahamu vigezo. Tunahitaji kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kila mwaka. Hilo ndilo jambo tunalopaswa kulifanya.
"Ni jambo la wazi kabisa, limejionyesha bayana kwa miaka ya karibuni kwamba tumekuwa na kikosi bora kinachotufanya tuwepo kwenye Top Four."
"Ni jambo la wazi kabisa, limejionyesha bayana kwa miaka ya karibuni kwamba tumekuwa na kikosi bora kinachotufanya tuwepo kwenye Top Four."
Subscribe to:
Comments (Atom)



















































