Tuesday, 2 July 2019

#SPORTS:Alexis Sanchez Kuwatolea Chafu Wanaomponda

Nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez kaibukana na kusema mbovu mbele ya watu wanaombeza juu ya kiwango chake katika ngazi ya klabu, maneno ya mchezaji huyo yamekuja baada ya kufanya vizuri katika michuano Copa America inayoendelea.
Alexis ameonyesha kiwango cha maana akiwa na kikosi chake cha Chile na ameifikisha timu katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.  
Mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota wa Chile ambao walipata penalti walipoingia muda wa matuta na Colombia kisha kuibuka kwa ushindi wa penalti 5-4 wikiendi.
Katika siku za karibuni, mchezaji huyo amekuwa na akizomewa kwa kufanya vibaya katika ngazi ya klabu.
Sanchez aliposti picha katika mitandao ya kijamii ikimwonyesha anashangilia huku akiwa kifua wazi na kusema; “Wanaongea upuuzi juu yangu, tazameni kiwango.”

No comments:

Post a Comment