Wednesday, 3 July 2019

#SPORTS:Messi Aonyeshwa Cha Moto Na Brazil

Nyota wa soka Lionel Messi kwa mara nyingine ameshindwa kuipa mafanikio timu yake ya Argentina baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali za michuano ya Copa America alfajiri ya leo.

Mechi hiyo ilichezwa hapo Bolo Horizonte na Brazil iakapata ushindi hivyo kungoja matokeo kati ya Chile na Peru ambazo zitacheza mechi ya nusu fainali alfajiri ya kesho.  Mabao yaliyowafanya Brazil watoke kifua mbele yalifungwa na Gabriel Jesus na Roberto Firmino.

Huenda suala la Messi kuipa timu yake ya Argentina taji la kimataifa likawa limeishia hapo hasa ikizingatiwa mchezaji huyo kwa sasa ana umri wa miaka 32.

 Pamoja na matokeo hayo Argentina watajilaumu wenyewe kwa kuwa walipiga mashuti 14 ya kulenga goli bila mafanikio.
"Tulitakiwa kufika fainali kwa kuwa tulistahili. Lakini wakati mwingine soka linakupa matokeo ambayo hukuyategemea,” alisema kocha wa Argentina Lionel Scaloni.

Rekodi ya Messi dhidi ya Brazil iko hivi; amecheza mechi 10, ameshinda tatu, amepoteza sita na sare moja.

No comments:

Post a Comment