Ratiba ya hatua ya mechi za mtoano, ama 16 bora ya Afcon tayari ipo wazi, na mwakilishi pekee wa Afrika Mashariki Uganda ataminyana na Senegal.
Senegal ambayo ilikuwemo kwenye kundi C pamoja na nchi mbili za Afika Mashariki, Kenya na Tanzania.Senegal ilizifunga timu hizo bila huruma; Tanzania 2-0 na Kenya 3-0
Uganda na Senegal zitashuka dimbani Ijumaa usiku na mshindi wa mechi hiyo atasonga mbele mpaka raundi ya robo fainali.
Katika mechi nyengine kali za hatua hiyo ya mtoano, miamba miwili ya soka barani Afrika, Cameroon na Nigeria wataumana jijini Alexandia siku ya Jumamosi.
Wenyeji Misri watakutana na Afrika Kusini, huku Ghana ikiminyana na Tunisia.
Ijumaa, Julai 5
Morocco vs Benin
Uganda vs Senegal
Jumamosi, Julai 6
Nigeria vs Cameroon
Misri vs Afrika Kusini
Jumapili, Julai 7
Madagascar vs DR Congo
Algeria vs Guinea
Jumatatu, Julai 8
Mali vs Ivory Coast
Ghana vs Tunisia

No comments:
Post a Comment