Klabu ya Chelsea itamuongeza pesa za maana Frank Lampard iwapo watamaliza msimu katika nne bora na kujihakikisha kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lampard atapata kiasi cha Pauni milioni nne kwa mwaka kwa kuinoa Chelsea, kiasi ambaco ni cha wastani ikilinganishwa na baadhi ya makocha katika Ligi Kuu England, lakini kocha huyo ataongezewa kiasi cha Pauni milioni moja kwa mwaka iwapo timu itakuwa ikipata nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Msimu uliopita, Chelsea ilipata bnafasi ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kazi ya Lampard ni kuhakikisha wanaendelea katika nafasi hiyo kila mara.
Chelsea wameanza kujiandaa kwa ajili ya msimu unaokuja lakini Lampard bado hajajiunga nao huku akitakiwa kutumia muda huo kumalizia baadhi ya mambo.


No comments:
Post a Comment