Wednesday, 3 July 2019

#SPORTS:Alichokisema Jesus Baada Ya Kumtoa Messi Machozi

Mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Jesus amesema baada ya mechi ya jana Jumanne iliyoisha kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Argentina katika nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Amerika Kusini (Copa Amerika), kuwa alijua angefunga bao.
Jesus alifunga bao la kwanza katika dakika ya 19 baada ya kupata pasi ya Roberto Firmino na dakika 19 kabla ya mchezo kuisha, akalipa fadhila kwa kutoa pasi ya bao la pili kwa mwenzake na kuiwezesha Brazil kufuzu kucheza fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007.
"Nilijisikia kuwa ningefunga. Sisema hilo kwa sababu nimefunga. Sikuwahi kusema hivyo katika mechi nyingine (zilizopita)," alisema mshambuliaji huyo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 22.
"Nilikuwa na uhakika sana... na niliweza kufunga kutokana na kiwango kizuri cha timu. Firmino alinipa pasi nzuri sana.
"Nimefurahi, si kwa sababu ya goli bali kwa ajili ya timu... Tulifunga mabao, wote tulifurahia mechi, jinsi tulivyojituma na kiwango.
"Lazima tucheze mechi zote kwa ari hii."

No comments:

Post a Comment