Baadhi ya watumiaji wa Facebook, Instagram na WhatsApp july 3 walishindwa kuweka picha, video na mafaili kwenye akaunti zao kutokana na tatizo la mtandao lililokuwepo.
Facebook, inayomiliki App zote tatu (Whatsapp,Instagram & Fb), imesema inafahamu kuhusu tatizo hilo na ilikuwa ''ikifanyia kazi ili kurudisha kila kitu sawa haraka iwezekanavyo''.
Washindani wake Twitter pia walikuwa na tatizo kwa watumiaji wake kushindwa kutuma ujumbe wa moja kwa moja au kupokea taarifa kuhusu ujumbe ulioingia.
Kampuni iliomba radhi kwa dosari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakisema kuwa wanashughulikia tatizo hilo.
Watumiaji bado waliweza kuweka ujumbe kwenye twitter na ujumbe wa hashtag #instagramdown ukaanza kushika kasi mtandaoni wengi wakitumia kueleza matatizo ya mshindani wake.
Tatizo limetokea kwenye baadhi ya kompyuta mama za data (Servers) zinazomilikiwa na Facebook ambazo zinahudumia huduma hizi zote tatu.
Kwa Tanzania tatizo lipo ingawa si ukubwa sana; ila tayari wapo ambao wanaathirika, tatizo kubwa limekuwa barani Ulaya na Amerika ya Kusini. Mitandao inayohusisha huduma za kutambua okosekaji wa huduma za kimitandao imeweza kutoa data ambazo zinaonesha mataifa yaliyoathirika zaidi;
Hii si mara ya kwanza na kwa huduma za kimtandao ni jambo ambalo hutokea, ila kwa Facebook inawezekana ikawa ni muda wa kujitazama na kufanya maamuzi ya kuboreshwa kwani ni mwezi wa tatu tuu huduma hizo tatu zilipitia matatizo haya haya.
Kwa kila dakika ambayo huduma hizi zinakuwa zinapata shida kampuni hiyo hupoteza mapato mengi kutokana na kushindwa kurusha huduma ya matangazo.
Kwa kila dakika ambayo huduma hizi zinakuwa zinapata shida kampuni hiyo hupoteza mapato mengi kutokana na kushindwa kurusha huduma ya matangazo.


No comments:
Post a Comment