Wednesday, 26 June 2019

Msanii Jaguar Toka Kenya Akamatwa Na Polisi Dhidi Ya Kauli Yake Kuwatisha Watanzania & Waganda (VIDEO)

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda waliopo jijini Nairobi.
Vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaripoti kuwa Charles Kanyi maarufu kama Jaguar amekamatwa mchana huu akiwa anatoka kwenye viwanja vya bunge.
Japo haijawekwa wazi kwa nini amekamatwa, tukio hilo linaunganishwa na kauli yake ya hivi karibuni kuhusiana na wafanyabiashara kutoka nchi jirani na kenya.
Katika kanda ya video iliosambazwa pakubwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini.
''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote'', alinukuliwa akisema.
Licha ya Serikali ya Tanzania kuwaomba raia wake kuwa na utulivu na serikali ya Kenya kujitenga na matamshi ya mbunge huyo, bado gumzo linaendelea katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtaka mbunge huyo aombe radhi kwa matamshi yake.
Soko kubwa la mitumba la jijini Nairobi la Gikombaa lipo ndani ya jimbo la Starehe.
Kituo Cha Kenya Citizen Imethibitisha Hilo

No comments:

Post a Comment