Friday, 28 June 2019
#SPORTSPep Guardiola Bado Ana Mpango Wa Kurudi Barcelona
Kocha wa Man City, 'Pep Guardiola' amesema kuwa bado ana mpango wa kurudi Barcelona siku moja.
Kocha huyo mwenye miaka 48, ambaye aliiongoza klabu ya Man City kupata vikombe vitatu msimu uliopita, amekuwa Etihad kwa miaka mitatu. Kocha huyo pia amepata ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili.
Kocha huyo mzaliwa wa Catalonia, ataingia msimu wa tatu akiwa na Man City na amebakiza miaka miwili katika mkataba wake.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona aliweka wazi kwamba anaweza kuongeza mkataba, lakini sasa ameibuka tena na kutamka, anatamani kurudi kwao na kuifundisha Barcelona kwa mara nyingine.
Siku za karibuni alitamka; "Nitakaa Man City kwa miaka miwili zaidi kama wananihitaji.Ninafurahia maisha hapa.”
Hata hivyo ameibuka upya na kutamka; “Nitarudi Barcelona hivi karibuni. Nimeshatembea klabu nyingine, nimefanya vizuri, nadhani bado ninahitajika Barcelona. Nitarudi huko.”
Labels:
Sports
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment