Kiungo wa Manchester City, David Silva ametangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu ujao na tayari kocha wake, Pep Guardiola anamtaka kiungo wa Real Madrid, Isco kuchukua nafasi ya staa huyo mwenzake wa Hispania.
Nafasi ya Isco au Francisco Roman katika kikosi cha Kocha Zinedine Zidane inatazamiwa kupotea zaidi baada ya klabu hiyo kuendelea kuwanunua mastaa wa nguvu kikosini lakini inaeleweka Guardiola ni shabiki mkubwa wa Isco.
Guardiola amekuwa akivutiwa na uwezo wa Isco tangu wakati alipokuwa akiifundisha Barcelona na kuna uwezekano mkubwa akatoa dau la kumchukua staa huyo wakati huu dau lake likizidi kushuka zaidi Santiago Bernabeu.
Kocha Zidane amemhakikishia namba Isco katika kikosi cha kwanza, hata hivyo Real Madrid itaipa uzito ofa yoyote ambayo itapelekwa kwao.
Hadi saaa Manchester City haijafanya usajili wowote mkubwa unaoweza kushtua na mipango ya Guardiola ni kutoa changamoto zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao.

No comments:
Post a Comment